Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama amewashauri madiwani wenzake kuangalia utaratibu na vigezo vitakavyofaa katika kuanzisha shule shikizi kwa lengo la kuwasaidia wananchi badala ya shule hizo kujengwa kiholela.
Mhe.Mhagama ameyasema hayo katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Amesema pawepo na utaratibu na vigezo ndani ya Halmashauri ambao utasaidia kuona namna gani kama kunauhitaji wa kujenga shule shikizi ijengwe na kutoa huduma kwa wananchi badala ya shule hizo kujengwa bila kufuata taratibu.
“Kuna maeneo yanauhitaji kuna maeneo ambayo wanachi wanaweza kwenda mashambani na kurudi na watoto wao wakaendelea na masomo katika shule mama”, amesisitiza Mhe.Mhagama.
Shule shikizi ni shule ambazo zinajengwa nje ya mfumo usio rasmi na wananchi wanaoishi mashamba mbali na makazi yao wakiwa na nia ya kufuata maeneo kwaajili ya kilimo.
Imeandaliwana kuandikwa na
JacquelenClavery
AfisaHabari Songea dc.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa