Ujenzi wa kituo cha afya Muhukuru.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea imepata shilingi milioni 500 kw ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Muhukuru
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw Simon Bulenganija ametoa taarifa hiyo katika kikao cha timu ya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya Halmashauri kilicho fanyika hivi karibuni ofisini kwake.
Bw Bulenganija amesema fedha hizo zimetolewa na OR_TAMISEMI_ AFYA mei 9 kwa ajili ya ujenzi wa majengo matano,kununua vifaa tiba toka bohari kuu ya madawa na uwekaji wa mifumo ya kisasa katika kituo hicho.
Ametaja majengo yanayotakiwa kujengwa ni jengo la kinamamama watotoato,chumba cha kuhifadhia maiti,chumba cha upasuaji na nyumba moja ya mtumishi.
Amesema katika kufanikisha na kukamilisha ujenzi huo tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa pamoja kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Muhukuru Lilahi ambako kituo kinajengwa na kuunda kamati ndogondogo za manunuzi,mapokezi na ujenzi na kila kamati imeshakabidhiwa majukumu yake.
Amezisisitiza kamati kutekeleza majukumu yake kwa uweledi mkubwa pamoja na kutunza kumbukumbu zote pia kujiepusha na kila aina ya ushawishi wa kuhujumu mradi huo bali wazingatie utaratibu ulio wekwa
Ujenzi huo utatumia muda wa siku 90 sawa na miezi mitatu kujengwakwake na kuanza kutoa huduma.Kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kutasaidia kutoa huduma kwa wananchi wa kata ya Ndongosi,kata ya Muhukuru Lilahi na mhukuru barabarani
Wananchi wameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh Raisi Dkt John Pombe Magufuli kwakuwajengea kituo cha Afya ambacho kitakuwa mkombozi kwao kwaupande wa huduma za afya na kuepukana na adha iliyokuwa ikiwapata mara baada ya kupata tatizo la kiafya
Imeandaliwa na.
Jacquelen Clavery.Habari,mawasiliano na mahusiano kazini.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa