Kufungwa kwa zahanati.
Serikali imetoa ufafanuzi juu ya kufungwa kwa zahanati za serikali kwakukosa watumishi na moja kugeuzwa kuwa duka la dawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Songea mh Pololeti Mgema katika kikao na waandishi wa habari cha kutoa ufafanuzi juu ya kufungwa kwa zahanati Kwa kukosa wa hudumu na kugeuzwa kuwa duka la dawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Mh Mgema amesema hakuna zahanati yoyote ya serikali iyofungwa katika Halmashauri hiyo wala majengo yake kugeuzwa kuwa duka la dawa katika vijiji vya Mdunduwalo,Lugagara na Litisha
Amesem vijjiji hivyo vilivyo tajwa bado vinaendelea na ujenzi wa zahanati baada ya kukamilika vitaanza kutoa huduma kama ilivyo katika zahanati nyingine kulingana na mwongozo wa serikali.
Imeandaliwa na jacquelen clavery.
Habari mawasiliano na mahusiano kazini
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa