Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (mst) Mary Longway amesema dhima ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni kuboresha taarifa zilizopo katika daftari hilo.
Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano mkutano wa wadau mbalimbali wa Uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma hivi karibuni
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji ( mst) Mary Longway amezitaja taarifa hizo kuwa ni Kurekebisha taarifa za wapiga kura,Kuhamisha taarifa za wapiga kura waliohama,Kuondoa taarifa za wapiga kura waliopoteza sifa na Kutoa kadi mpya kwa wapiga kura kwa waliopoteza au kadi zao kuharibika pamoja na kuandikisha watu wenye umri wa miaka 18 na wale ambao watakua wametimiza umri wa miaka 18 siku ya Uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Jaji ( mst) Longway amezitaja sifa za kuandikishwa kuwa mpiga kura kuwa ni awe raia wa Tanzania, awe na umri wa miaka 18 na zaidi au atatimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya Uchaguzi.
Amesema raia yeyote wa Tanzania atapoteza sifa za za kuandikishwa kuwa mpiga kura kwa sababu zifuatazo si raia wa Tanzania, anautii wa nchi nyingine,amethibitika kuwa anaugonjwa wa akili,amehukumiwa adhabu ya kifo,anatumikia kifungo cha zaidi ya miezi sita sababu nyingine ni amezuiliwa kujiandikisha ni kuwa mpiga kura na sheria ya uchaguzi au sheria nyingine kuwa makosa yanayohusiana na uchaguzi au hakutimiza umri wa kupiga kura ifikapo siku ya uchaguzi.
Ameyataja maeneo ambayo hayatahusika kuwa vituo vya uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi sura ya 343 na kanuni ya 15(3) ya kanuni za Uboreshaji wa daftari chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa Sura ya 292 kuwa ni Kambi za jeshi, Nyumba za ibada,ofisi za vyama vya siasa na makambi na makazi ya polisi.
Kwa Mkoa wa Ruvuma zoezi la uandikishwaji wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura litaanza tarehe 30.12.2019 hadi tarehe 05.01.2020 kwa muda wa siku saba na vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni kwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya zoezi hilo hivyo wananchi wanatakiwa kwenda kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha.
Kwa upande wa wananchi wametoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa na ofisi ya Tume ya Uchaguzi ngazi ya Mkoa ili taarifa ziboreshwe mara kwa mara sio kwa kipindi fulani tu ambacho kinaonekana kuto kidhi matakwa ya wananchi kwani muda unakua ni mchache.
JACQUELEN CLAVERY-AFISA HABARI.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa