Imebaika kuwa utoro wa kudumu,uhaba wa vitendea kazi ,uhaba wa vyumba vya madarasa ni miongoni mwa changamoto zinazoikabibili sekta ya Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Hayo yamebainishwa na walimu pamoja na wadau wa Elimu, kufuatia ziara iliyofanywa na uongoziwa idara ya Elimu katika kata zote 16 za Halmashauri ya Wilaya Songea kwa lengo la kufanya tathimini ya Elimu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Walimu na wadau wa Elimu wamesema utoro,uhaba wa vitendeakazi,na vyumba vya madarasa ni miongoni mwachangamoto zinayoikabili sekta ya Elimu nakupelekea matokeo hasi ya mitihani ya darasa la saba mwaka 2017.
Wametaja sababu nyingine pamoja na mwamko hafifu wa wazazi kufuatilia maendeleo ya Elimu kwa watoto wao,kipindi cha masika wazazi kuhamia mashambani na watoto,na kusababisha wanafunzi kuto hudhuria masomo ipasavyo, uhaba wa walimu, na uzembe wa baadhi ya walimu wa kutohudhuria vipindi madarasani.
Kufuatia changamoto hizo Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw TANU KAMEKA kwa kushirikiana na wataalamu wengine wa Elimu wameahidi kufutilia matatizo hayo nakuyatolea ufumbuzi kwakufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa mara kwa mara mashuleni.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa