MKURUGENZI wa TASAF kutoka makao makuu Dodoma Ladslaus Mwamanga ambae amewakilishwa na Mercy Mandawa ametoa mafuzo na kuwajengea uelewa juu ya utekelezaji na usimamizi wa miradi ya TASAF Songea.
Mafunzo hayo yamefanyika kwenye baraza la Waheshimiwa Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea katika ukumbi wa mikutano Peramiho.
Pia amewapongeza Waheshimiwa Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri kwa kwa uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa shughuli za mradi kwa weredi na ufanisi mkubwa tangu hatua za mwanzo hadi kukamilika.
‘’Mradi unapoandaliwa vizuri, kutekelezwa na kusimamiwa kwa utaratibu uliopangwa thamani ya fedha iliyotumika itapatikana na malengo yaliyokusudiwa yatafikiwa’’, amesema Mercy Mandawa.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Menace Komba ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kwa kuendelea kuikimbuka Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe amesema mafunzo haya wezeshi yatasaidia viongozi wa siasa na wataalamu katika kusimamia miradi ya Ajira ya muda na uendelezaji wa miundombinu.
Pia Katibu tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Daniel Ndumbaro amewashauri waheshimiwa Madiwani na wataalamu wa Halmashauri kile walichojifunza wakifuatilie wafate taratibu na kanuni katika uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa shughuli za mradi wa TASAF wakifuata miongozo iliyowekwa.
TASAF ni mradi wenye lengo la kusaidia watu wanaotoka katika kaya maskini, kutoa Ajira ya muda kwa walengwa ili kuongeza kipato na matumizi kwenye kaya na kuongeza ujuzi kwa walengwa.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni,
Kitengo cha Mawasiliano Serikali.
Septemba 02 2022.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa