AWAMU ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) inatarajia kuzifikiakaya masikini zaidi ya milioni 1.4 zinazokadiriwa kuwa na watu zaidi ya milionisaba kote nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga wakatianafungua mafunzo ya siku sita ya timu maalum ya wawezeshaji 25 kutoka Halmashauriza Madaba na Songea wilayani Songea yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Ushirikamjini Songea.
Mwamanga amesema wawezeshaji hao watahusika na utekelezaji na usimamizi wamiradi ya kutoa ajira za muda kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikiniTASAF Awamu ya tatu katika kipindi cha pili.
“Miradi ya kutoa ajira za muda inalenga kutoa ajira kwa kaya masikini wakatiwa kipindi cha hari ili wanakaya hao wasiweze kuuza rasilimali walizonazo kwaajili ya kupata fedha na kuwezesha ajira kwa kaya ili kuongeza kipato hivyokupunguza umaskini’’,alisema.
Hata hivyo amezitaja kaya zitakazoshiriki utekelezaji wa miradi hiyo nizenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi na wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi65.
Mwamanga amesema katika kipindi cha kwanza cha mpango wa kunusuru kayamasikini jumla ya miradi 9,440 ya kutoa ajira za muda ilitekelezwa kwagharama ya shilingi bilioni 1.19 kati ya hizo shilingi bilioni 83.3 zilitumikakwa kulipa ujira wa walengwa na shilingi bilioni 35.7 kwa ajili ya vifaa vyamiradi na usimamizi.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka TASAF Makao Makuu FrankAntony amelitaja lengo la mafunzo hayo kuwa ni kujenga uwezo wa timu zawatalam ngazi ya Halmashauri za Songea na Madaba kuhusiana nauibuaji,uandaaji,utekelezaji na usimamizi miradi ya kutoa ajira za muda kwawalengwa ngazi ya jamii.
Amesema mafunzo hayo ya nadharia na vitendo ya siku sita ambayo yametolewakwa wawezeshaji 25 toka Halmashauri mbili za Madaba na Songea yatawapelekeamaarifa jumla ya walengwa wa TASAF 5,400 kati yao walengwa 3,800 tokaHalmashauri ya Songea na walengwa 1,600 toka Madaba.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa