Hayo ameyasema Waziri wanchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapt George Mkuchika (mstaafu) alipofanya ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na TASAF na kuzungumza na walengwa wa kaya masikini katika Kijiji cha Matimira Kata ya Matimia,Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruuvuma hivi karibuni.
Kapt Mkuchika (mstaafu) amesema Serikali imeadhimia kuzifikia kaya zote maskini nchini kwa lengo la kuwanusuru na maradhi, ujinga na umaskini ambao ni maadui wakubwa wa mafanikio katika jamii.
Amesema jambo la kutia moyo kwa wananchi kuona Serikali inapotoa fedha kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini walengwa wanatumia fedha hizo kwa kujiongezea kipato kwa kufanya kazi za kiuchumi kama vile ufugaji,kilimo hata uvuvi na kugharamia huduma za matibabu na Elimu.
Amewatoa hofu walengwa wa kaya masikini kuwaTASAF inasimamiwa na serikali hivyo walengwa wataendelea kunufaika na mpango huo kwa kuzingatia taratibu na miongozo iliyopo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bibi Christina Mndeme amesema atasimamia fedha zote zinazotolewa na Serikali kwa lengo la kunusuru kaya masikini zinafanya kazi iliyokusudiwa.
Aidha Halmashauri ya wilaya ya songea inajumla ya kaya masikini 145, kaya moja ikiwa imehama na kubakiwa kaya 144 sawa na asilimia 96 zinazohudumiwa kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini kati ya kaya 151 zilizo tambuliwa na kaya sita hazikukidhi vigezo.
Kwa upande wao wananchi wameishukuru serikali kwakuwanusuru na maisha magumu waliyokuwa wakiyapitia kwakuwasaidia fedha ambazo wameweza kuanzisha miradi midogomidogo ya kiuchumi ambayo imeinua kipato cha maisha na kuboresha makazi yao.
JACQUELEN CLAVERY-TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa