Mfuko wa maendeleo ya jamii, TASAF, umeanza kuwalipa fedha wananchi wa kaya maskini katika halmashauri ya wilaya ya Songea.
Huu ni mpango wa Selikari katika kunusuru kaya Maskini ikiwemo kuwaongezea kipato na kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii kwa kwa kaya za waklengwa na kulinda masahi ya Watoto wao.
Lengo la Serikali ni kuwakwamua katika hali ya chini ili mpande na muwe na uwezo wa kujitafutia na kusaidia kaya zenu. Mama Samia anawapenda wananchi wake ndo mana ameamua kuwapatia fedha hizi ili wananchi wake muweze kupata mahitaj ya muhim ikiwemo kupeleka watoto Shule na kuanzisha miradi mbalimbali ambayo itawasaidia katika familia zenu. Alisema Mratibu wa TASAF Mkoa Wa Ruvuma akiongea na walengwa katika kijiji cha Morogoro na Magima kata ya Litisha
Aidha aliwataka walengwa kuheshimu fedha hizo wanazopewa na kuwasisitiza kuzipeleka kwenye mambo ya Msingi ambayo yanaweza kusaidia kwa sasa na baadae. Leo mmeona wenzenu wakua wanufaika wa TASAF kwa miaka zaidi ya Tisa ( 9 ) wapo ambao wamejikwamua kwa kuweza kujenga nyumba zao, na kusomesha watoto wengine waneanzisha miradi ambayo kwa sasa wameweza kusimama wenyewe,
Hivyo basi wito wangu kwenu ni kuhakikisha mnakua na mipango madhubuti ili kuendeleza familia lakini pia kumpa moyo Mhe. Rais ambaye amekua akitoa fedha hizi kwa ajili yenu.
Wanufaika wa mfuko wa Maendeleo ya Jamii ( TASAF), wamemshukuru sana Mhe. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKt samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka kaya maskini lakini pia kuwakwamua kutoka Kwenye Umakini
“ Kiukweli sisi kaya Maskini, tunamshukuru sana Mama Samia, ametupa unafuu wamaisha ametupa, mwanzo nilikua namaisha magumu sana, lakini kwa sasa nimeanzisha biashara yangu nauza kanga na yote hii ni fedha ninayoipata kupitia TASAF.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa