TAKUKURU yavitahadharisha vikundi vya wanawake,vijana na walemavu
Mkuu waTAKUKURU wa Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda amevitahadharisha vikundi vya wenyeulemavu ,wanawake na vijana ambavyo vimenufaika na mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri za Wilaya na Manispaa kurejesha mikopo kulingana na mikataba yao.
Mwenda ametoa kauli hiyo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa kazi za TAKUKURU kwa kipindi cha robo cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2020 kwa waandishi wa Habari leo katika ofisi ya TAKUKURU Mjini Songea.
Mwenda amevitahadharisha vikundi vya wanawake ,vijana na wenye ulemavu ambavyo vimepata mikopo inayotolewa na Halmashauri za Wilaya na manispaa kurejesha fedha hizo kulingana na makubaliano lasivyo takukuru haita waacha salama kwakuwachukulia hatua za kisheria.
“Mkopo siyo hisani TAKUKURU itamfuatilia mtu mmoja mmjo katika kufuatilia fedha za serikali”,amesema Mwenda
Amesema uchunguzi uliofanywa na Taasisi hiyo umebaini baadhi ya vikundi siyo endelevu viliundwa kwa lengo la kuchukua mikopo na baada ya kukopeshwa vimesambaratika na walipotakiwa kuonyesha miradi wanayojihusisha nayo walionyesha miradi ya vikundi vingine.
Ameongeza kwa kusema kwa kipindi cha muda huo Taasisi imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 50 kutokana na dhuluma mbalimbali kutoka kwenye vyama vyama vya ushirika (AMCOS),vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) Makampuni binafsi yanayojihusisha na ukopeshaji fedha dhuluma zinazofavywa na baadhi ya walezi, mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa na safari hewa za wakuu wa Idara kwenye baadhi ya halmashauri za wilaya.
Akizungumzia kuhusu kuwafikishia wananchi huduma katika makazi yao,TAKUKURU imeanzisha huduma ya kuwatembelea wananchi kwa mwezi mara moja kwalengo la kusikiliza na kutatua changamoto zao badala ya wanachi kufuata huduma katika ofisi za Taasisi hiyo kwa kutoa matangazo ya siku ambalo watalitembelea.
Mwenda anaendelea kutoa wito kwa wananchi na wadau wote wa kupinga kupambana na kuzuia rushwa kushirikiana katika mapambo dhidi ya rushwa ,kwani rushwa ni adui wa haki na inasababisha madhara makubwa ikiwemo kifo.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavvery
Afisa Habari Songeadc
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa