MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe anawatangazia wananchi wote kuwa Halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 149,934,332 kupitia Ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tanzania Education Authority- TEA) kwaajili ya ujenzi wa bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 120.
Pia amesema Halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 362.2 kutoka katika kampuni ya Barrick Gold Mine Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari Maposeni.
Ndugu Neema amesema fedha hizo zitatumika kujenga madarasa manne ambapo kila darasa litagharimu shilingi milioni 24 na kufanya jumla shilingi milioni 96 kwa madarasa manne, mabweni mawili ambapo kila bweni litagharimu shilingi milioni 128 na kufanya jumla shilingi milioni 256 kwa mabweni mawili na mwisho ujenzi wa matundu ya vyoo sita ambapo kila tundu litagharimu kiasi cha shilingi milioni 1.7 na kufanya jumla ya shilingi milioni 10.2 kwa matundu sita ya vyoo.
Aidha, amesema kampuni ya Barrack wametoa fedha hizo ili kuunga mkono jitihada na juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha elimu nchini.
Ameongeza kuwa lengo la ujenzi wa miundombinu hii ni kuwezesha wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha tano mwaka 2023, wanapata fursa ya kuendelea na masomo.
Vilevile amesema Halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 834 kutoka Serikali kuu kwaajili ya kuongeza miundombinu ya wanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari Jenista Mhagama.
Ndugu Neema amefafanua kuwa fedha hizo zitatumika kujenga madarasa 12 ambapo kila darasa litagharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 24 na kufanya jumla ya shilingi milioni 288 kwa madarasa yote 12, mabweni manne ambapo kila bweni litatumia fedha kiasi cha shilingi milioni 128 na kufanya jumla ya milioni 512 kwa mabweni manne na ujenzi wa matundu ya vyoo 20 ambapo tundu moja litagharimu shilingi milioni 1.7 na kufanya jumla ya shilingi milioni 34 kwa matundu 20 ya vyoo.
Pia amesema Halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 751.8 kutoka Serikali kuu kaajili ya kuongeza miundombinu ya wanafunzi wa kidatocha tano katika shule ya sekondari Mpitimbi.
Ndugu Neema amefafanua kuwa fedha hizo zitatumika kujenga madarasa tisa ambapo kila darasa litagharimu shilingi milioni 24 na kufanya jumla ya shilingi milioni 216, mabweni manne ambapo kila bweni litagharimu shilingi milioni 128 na kufanya jumla ya shilingi milioni 512 kwa mabweni manne na ujenzi wa matundu ya vyoo 14 ambapo tundu moja litagharimu milioni 1.7 na kufanya jumla ya milioni 23.8 kwa matundu ya vyoo 14.
Kwaniaba ya Uongozi wa Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Neema ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Joakim Mhagama kwa kuendelea kuimarisha miundombinu ya elimu.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa