Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amesema Wilaya ya Songea inatarajia kukamilisha ujenzi wa madarasa yote 10 yanayogharimu kiasi cha shilingi Milioni 200 ifikapo Novemba 30 mwaka huu.
Akizungumza na Menejimenti ya Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Songea,Mheshimiwa Mgema amesema ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari unaendelea vizuri ambapo wanatarajia kumkabidhi madarasa yote Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ifikapo Desemba 10 mwaka huu.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa