HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea imepokea kiasi cha shilingi milioni 396,141,283.61 kutoka TASAF kwaajili ya ujenzi wa miradi ya miundombinu kwa mwaka 2022/2023.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe katika mkutano uliohudhuriwa na wataalamu na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano peramiho.
Aidha amesema kiasi cha shilingi milioni 225,145,486.29 zitatumika katika ujenzi wa kituo cha magari katika kijiji cha Parangu.
Pia kiasi cha shilingi 170,995,797.32 zitatumika katika ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa zahanati ya Mdunduwalo pamoja na uchimbaji wa kisima cha maji cha Mdunduwalo.
‘’Napenda kutoa shukrani za dhati kwa serikali yetu ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mbunge wetu wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kwa kutuletea fedha zinazotusaidia katika shughuli za kuijenga Halmashauri yetu’’, amesema Ndugu Neema.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Menace Komba ametoa rai kwa wataalamu kufanya kazi kwa weredi na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa wananchi kwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Nae Mratibu wa TASAF wa Wilaya Hossana Ngunge ameahidi kuhakikisha fedha hizo anazisimamia kwa ufanisi mkubwa ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Agosti 31 2022.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa