Naibu Waziri wa Elimu TAMISEM David Silinde amehaidi kuendelea kusimamia ujenzi wa miundombinu ya elimu kwalengo la kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia.
Silinde ametoa ahadi hiyo alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia mradi wa Mpango wa maendeleo wa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea hivi karibuni
Silinde amesema ataendelea kusimamia na kuhakikisha miundombinu ya kutolea elimu inajengwa na mazingira ya kujifunzia na kufundishia ya na kuwa bora na mazuri kwa walimu na wanafunzi.
“Mimi ni mkali lakini kwa miradi hii napongeza”,amesisitiza Silinde
Silinde amewapongeza viongozi na wadau walioshiriki kutekeleza ujenzi wa vyumba hivyo kwa kuzingatia maagizo na maelekelezo yaliyotolewa na serikali kwakwenda na muda wa ukamilishaji wa miradi hiyo.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Neema Maghembe amesema jumla ya vyumba vya madarasa 65 vimejengwa na kukamilika kati ya hivyo vyumba 46 vimejengwa kwenye shule za sekondari zote za Serikali ambazo ni 16,madarasa 19 yamejengwa kwenye vituo shikizi vya shule za msingi tano.
Ameongeza kwakusema wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022 hakuna atakayebaki nyumbani kwakigezo cha kukosa vyumba vya madarasa wote wataanza masomo kulingana na taratibu,sheria, kanuni na miongozo ya nchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea ilipata mgao wa fedha toka Serikalini jumla ya shilingi Bilioni 1.3 kwaajili ya kujenga vyumba 65 vya madarasa na kila darasa limegharimu shilingi miloni 20 pamoja na madawati yake kwa shule shikizi za msingi ,meza na viti kwa upande wa sekondari.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa