Siku ya wazee Duniani huadhimishwa tarehe 01 Oktoba ya kila mwaka kwa ajili ya kukumbushana umuhimu wa wazee ili waweze kuwa na maisha bora yenye kuleta matumaini aidha wanapokuwa wamestaafu au wanapokuwa na umri mkubwa.
Siku ya Wazee Duniani ilitengwa mwaka 1990 katika Azimio namba 45/106 la mwaka 1990 .baada ya mkutano mkuu wa umoja wa mataifa kuamua rasmi kuanzisha siku hii.
Nchini Tanzania idadi ya wazee inatajwa kuwa kubwa zaidi kuliko watoto chini ya miaka 15. Kwa mujibu wa takwimu za karibuni, Duniani kufikia mwaka 2050 karibu asilimia 21 ya watu wa sasa watakuwa ni wazee.
Hivyo kupitia siku hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Songea kupitia kitengo cha Ustawi wa jamii imeandaa maadhimisho hayo ambayo yanatarijiwa kufanyika Tarehe 29 Septemba katika Kijiji cha Nakahuga Kata ya Litisha ambapo maadhimisho hayo yatatanguliwa na kongamano la wazee ambalo litafanyika siku moja kabla ya Kilele cha maadhimisho hayo. Ambapo amesema,
"Kuelekea kwenye Kilele cha maadhimisho haya ambayo kwa Wilaya ya Songea tutafanya tarehe 29 septemba kutokana na muingiliano wa ratiba hivyo tumeandaa vitu mbalimbali vitafanyika siku kabla ya Kilele na siku ya Kilele kwa kuanza na siku ya Tarehe 28 kutakuwa na kongamano la wazee ambalo litajumuisha vitu vifuatavyo Elimu yaukatili wa kijinsia ili kuwawezesha wazee kutoa taarifa pale wanaponyanyaswa, Elimu ya lishe Bora, Elimu ya Utunzaji wa mazingira na afya pamoja na Elimu ya kifua kikuu na ukoma"
"Vilevile siku ya Kilele kutakuwa naupimaji afya kwa wazee (Kupima shinikizo la damu kisukari, uchunguzi wa kifua kikuu na ukoma), pia kutakuwa na maonesho ya shughuli za kiuchumi zinazifanywa na wa wazee wazee kama vile kilimo, ufugaji wa kuu na kilimo cha uyoga, pia kutakuwa na maonesho ya ngoma za asili(Lizombe) ya wazee na watoto, kutakuwa kukimbiza kuku, kuvuta kamba na mpira wa miguu wa wazee" Alisema Joseph Ngwenya Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea
Hivyo ametoa wito kwa wananchi wote wa Kijiji cha Nakahuga Kata ya Litisha na majirani wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku ya Kilele ambayo maadhimisho hayo yataanza sa 2 asubuhi yakiongozwa na Kaulimbiu isemayo "UTHABITI WA WAZEE KWENYE DUNIA YENYE MABADILIKO" na mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe.Wilman Kapenjama Ndile.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa