Shule ya Sekondari Mtopesi iliyopo katika kijiji cha Lugagara kata Kilagano, imeanza kupoea wanafunzi wa kidato cha kwanza Sabini na moja (71) mwanzoni mwa mwaka 2024
Tarehe 30/08/2023. Shule ya Sekondari Mtopesi, ilipokea kiasi cha shilingi TZS. 560,553,827 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika kijiji cha Lugagala kupitia mradi wa kuboresha elimu ya sekondari ( SEQUIP)
“ katika fedha hizo tulitakiwa kujenga jingo la utawala, madarasa nane maabara tatu yaani Fizikia, Kemia na Bailojia jengo la Tehama, Maktaba pamoja na vyoo. Hatua iliyofikia ujenzi umekamilika kwa maana madarasa yamekamilika na wanafunzi wameanza masomo.”
Tunaishukuru sana Serikali Mhe Rais maana kabla ya shule hii watoto kutoka kijiji cha Lugagara, Zomba na Mwimbasi walitakiwa kwenda kusoma Sekondari ya Kilagano ambayo ipo km 15 kutoka hapa, kiukweli wanafunzi walikua wanatembea umbali mrefu sana, lakini kwa kupata Sekondari hapa kimesaidia sana wanafunzi kupata masomo kwa urahisi.” Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtopesi
Betrice Raphaeli Komba, ni mkazi wa kijiji cha lugagara kata ya Kilagano naye ana haya ya kusema “kwanza tunashukuru sana Serikali kwa Kujenga hii shulenya Mtopesi, changamoto ya mwanzoya mwanzo watoto walikua wanasoma mbali kwa kipindi cha mvua kama hivi walikua wanapata tabu sana lakini kwa sasa tunashukuru sana
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa