Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, inampango wa kutengeneza masoko ya zao la Mahindi ndani nan je ya Nchi hivyo kuwataka wananchi kutouza chakula kwa Madalali.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, ( Sera Bunge na Uratibu) Mhe Jenista Joakim Mhagama, wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kizuka iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Hii ni baada ya wananchi kuendelea kuuza mahindi kiholela tena kwa bei ya chini ambayo haiweza kurudisha gharama walizotumia katiaka kuandaa zao hilo.
“Hongereni, Mvua zilikua kubwa , Barabara zimeharibika ila wananchi mmepata mahindi ya kutosha. Uzeni kwa utaratibu, uzeni kidogo saivi subirini utaratibu utakaopangwa na serikali. Serikali imeweka utaratibu, Mhe Rais ametafuta Masoko la Mahindi ndani na nje ya Nchi, hivyo tutaweka utaratibu ili tuweze kuuza kwa utaratibu mzuri ambao utawawezesha kupata faida.
Aidha Mhe Jenista aliwataka wananchi wasiuza chakula chote kwa sababu ya tama ya fedha “ hata hivyo nawaomba msiuze chakula chote, achene chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi ya familia
Hata hivo Mhe Jenista aliwataka pia wananchi kuzingatia Lishe bora wa watoto wao wazazi wahakikishe watoto wanapata chakula tofauti sio ugali nyama tu kila siku
“ Katibu tawala amesisitiza hapa, Mkiacha chakula cha kutosha kwa ajili ya Lishe bora, Watoto wetu wanahitaji lishe bora, tuwachanganyie vyakula tofauti ili kuhakikisha wanapata Afya Bora”
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa