Shilingi milioni 210 zimetumika kutoa ruzuku kwa kaya masikini katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Afisa Tehama kutoka makao makuu ya TASAF Peter Lwanda amesema hayo katika zoezi la kutoa ruzuku kwa kaya masikini zoezi lililo fanyika hivi karibuni.
Lwanda amesema jumla ya kaya masikini 3249 ambazo ni ruzuku ya mwezi wa Julai hadi Agasti na Septemba hadi Oktoba 2020.
Amesema wamelazimika kutoa ruzuku ya miezi minne kutokana na changamoto ya ugonjwa wa COVID 19, sababu iliyopelekea walengwa kutopatiwa ruzuku hiyo kwa muda uliotakiwa ambao ni kila baada ya miezi miwili.
Lwanda amesema katika kipindi cha miaka minne iliyoanza 2020,mpango wa kunusuru kaya masikini umelenga kukuza uchumi wa kaya masikini katika sura mbili.
Amesema katika sura ya kwanza ni kutoa ruzuku kwa kaya ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi kama wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 65 au makundi maalumu.
Katika sura ya pili TASAF itawasaidi walengwa ambao wanauwezo wa kufanya kazi kwakuwajengea uwezo wakuwapa mafunzo ya ujasiriamali kupitia vikundi vya watu 10 hadi 15 na kuwaunganisha na Taasisi za kifedha ili waweze kupatiwa mikopo na kuendeleza shughuri zao ,hali kadharika kutoa ajira za muda za miradi ya TASAF na kulipwa ujira.
“Nasitiza walengwa kutumia fedha vizuri pamoja na kuhakikisha watoto wanaopata ruzuku wanahudhuria shuleni”,amesema Lwanda.
Domitila Mhagama na Agustino Soko ni wa kazi wa kijijij cha Litapwasi wamesema tangu waanze kupata ruzuku Maisha yao yameimarika kiuchumi kwa kujenga nyumba bora,kufanya shughuri ndogo ndogo za ufugaji kilimo na uhakika wa kupata chakula kwa mwaka mzima katika familia zao.
Wameishukuru serikali kwakuona tatizo la kaya masikini na kuwapa ruzuku ambayo inawasaidia kutatua changamoto kutokana na ruzuku wanayoipata.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery -Afisa Habari Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa