MKUU wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kiasi cha shilingi milioni 848 kujenga mradi wa maji katika Kijiji cha Parangu kilichopo Kata ya Parangu,
Mgema ameyasema hayo wakati akikabidhi miundo mbinu ya ujenzi wa miradi ya maji katika kijiji hicho kwenye hafla fupi iliyofanyika hivi karibuni katika Shule ya Sekondari ya Jenista Mhagama iliyojengwa katika kijiji hicho.
“Napenda nitumie fursa hii kumpongeza Rais wetu Mhe.Samia Suluhu Hassani kwakutupa fedha nyingi katika Wilaya yetu ya Songea katika sekta zote za ujenzi wa miradi,”amesema Mgema.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Menas Komba amemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Jenista Mhagama kwa ufuatiliaji wa fedha kutoka Serikali kuu ambazo zinatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kushirikiana na viongozi na wadau wengine wa maendeleo
.
Mhe.Komba amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya kazi kubwa katika kuwaletea wananchi maendeleo kusudiwa kulingana na ilani ya Ccm ya mwaka 2020-2025 na kwamba kazi kubwa hivyo wao kama viongozi jukumu lao ni kusimamia fedha zinazotolewa na Serikali zinatekeleza ujenzi wa shughuli za miradi kama ilivyokusudiwa.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bernadetha Mapunda ameishukuru Serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Mijini na Vijijini(RUWASA ) Songea kwa kuwajengea mradi huo wa maji ambao utawasaidia kuokoa muda wa kufuata maji umbali mrefu kwenye visima vya asili, pia utawaondolea maradhi yatokanayo na maji yasiyosafi na salama
Mapunda amesema kupitia mkutano wa hadhara walioketi wameadhimia kumtia hatiani mtu yoyote atakayebainika anaharibu vyanzo vya maji na atakayekaidi kuchangia gharama za huduma za maji ambazo ni shilingi 2000/= kiwango ambacho wamekubaliana
Aidha Meneja wa Ruwasa wilaya ya Songea Mhandisi Mathias Charles amesema mradi huo wa kijiji cha Parangu utajengwa umbali wa kilometa 19.55 ambapo kukamilika kwake utahudumia wananchi wapatao zaidi ya 3,000 na kwamba mradi huo umeanza kujengwa na utakamilika ifikapo mwezi juni 2022
Mhandisi Charles amewasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa kupanda miti kwenye vyanzo vya maji, kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya vyanzo vya maji kwani shughuli hizo zinaathiri vyanzo hivyo
Ameitaja miradi mingine ambayo inatekelezwa na Ruwasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea kuwa ni mradi wa maji Mtiririko wa Matimira na Mpitimbi B kwa jumla ya gharama ya bilioni 1.6
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songea dc
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa