Ofisi ya Takukuru Mkoani Ruvuma imeokoa kiasi cha shilingi milioni ishirini na tano kutoka idara ya Afya na Elimu.
Hayo yamesemw na mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa BI CHRISTINA CHAKAGA wakati akitoa taarifa ya utendaji wa kazi kwa kipindi cha miezi 9 kuanzia mwezi aprili hadi Desemba 2017 kwa waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni.
Bi Chakaga amesema kiasi hicho cha fedha zimeokolewa kutoka idara hizo kama mishahara hewa kwa baadhi ya watumishi.
Bi chakaga ametaja maeneo yanayo lalamikiwa kwa vitendo vya rushwa ni idara ya ardhi, mahakama, kilimo,polisi, vyama vya siasa,Elimu na TAMISEMI.Pia utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa maji,barabara na badhi ya vituo vya Afya isiyo kamilika kwa wakati.
Adha Bi chakaga ametoa wito kwa wananchi kushiriki katika mikutano yote inayo itishwa na vyombo vyenye mamlaka kwa lengo kupata taarifa na maagizo mbalimbali yanayo tolewa na vyombo hivyo.
Taasisi ya kuzuia na kupambana Rushwa nchini inafanya kazi kwa mujibu wa sheria namba 11 ya mwaka 2007.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa