Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Balozi Wilbert Ibuge amewataka viongozi mbalimbali wa Taasisi na wadau wa Afya kuongoza kwa vitendo na kwamfano katika kusimamia miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya juu ya umuhimu wa chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa UVICO wimbi la tatu.
Balozi Ibuge ametoa maagizo hayo katika uzinduzi wa chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa UVICO uliofanyika katika ukumbi wa manispaa ya songea leo.
Balozi ibuge amewataka viongozi mbalimbali wa taasisi na wadau wa afya kushirikiana katika kujenga uelewa wa kutosha kwa wananchi ili watambue umuhimu wa kujikinga na janga hilo kwa kuchanja chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa UVICO wimbi la tatu.
Balozi Ibuge amesisitiza kwakusema chanjo iliyotolewa na Serikali ni chanjo salama kwa kila atakaye penda kuchoma na nia ya serikali ni kuokoa wananchi wake ili wasiweze kuangamia na ugonjwa huo ,hivyo wananchi wajiepushe na uzushi wowote wa kwenye mitandao ya kijamii inayodai chanjo hiyo inamadhara.
Amesema Serikali kupitia Wataalam wa Afya wamekuwa wakitoa elimu na maelekezo mbalimbali kuhusu athari za ugonjwa wa UVICO ambao umekuwa tisho kwa uhai wa mwanadamu,nivema wananchi pasipo shuruti waone umuhimu wa kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.
Balozi Ibuge amekili kuwepo kwa wagonjwa ndani ya mkoa wa Ruvuma hivyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari binfsi badala ya kuwasubiri viongozi kuwahamasisha na kuwakumbusha kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
“Msisitizo wangu kujinga ni bora zaidi kuliko kujitibia “,alisisitiza Balozi Ibuge.
Amepiga marufuku mikusanyiko yote isiyo kuwa ya lazima huku akitoa maagizo kwa kamanda wa polisi wa mkoa ahakikishe kwenye vyombo vya usafiri wa umma abiri wote wanavaa barokoa na hakuna abiria kusimama na boda boda kupakia abiri mmoja.
Maagizo mengine ni viongozi wa idara ya afya kuhakikisha vifaa kinga vinapatikana katika mikusanyiko ya watu kama sokoni,standi za mabasi na maeneo mengine ambayo watu wanakusanyika kwa ajili ya shughuli zao za kila siku.
Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Jairoy Khanga amesema Mkoa wa Ruvuma umepokea jumla ya chanjo 30,000 ambazo zimesambazwa katika vituo 23 ndani ya Mkoa ambako wananchi ambao wamehiari kwenda kuchanja watapata huduma katika vituo hivyo.
Ikumbukwe kuwaugonjwa wa UVICO ulingia nchi Marchi 17,2020 ambapo bado ugonjwa huo umekuwa hatari duniani kwa kuteketeza uhai wa mwanadamu kwa kipindi kifupi na mapambano bado yanaendelea kupitia wataalam mbalmbali wa Afya Dunia kuhakikisha ugonjwa huo hauangamizi msMaisha ya watu .
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa