Rc Mndeme na maagizo 20 ya kuukabili ugonjwa wa corona
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametoa maagizo 20 ya kukakabiliana na ugonjwa wa corona Mkoani Ruvuma .
Mndeme ametoa maagizo hayo katika kikao cha kamati ya maafa ya Mkoa na Wilaya kujadili mbinu na mikakati ya kukabiliana na janga la ugonjwa wa corona kilicho fanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Baadhi ya maagizo hayo ni Wakuu wa Wilaya wote kuzuia mipaka yote ambayo siyo rasmi kwa lengo la kudhibiti uingiaji na utokaji holela wa wageni.
kukagua maduka kwania ya kubaini bei za vifaa vya kujikinga na maabukizi ya virus vinavyosababisha ugonjwa wa corona kama vinauzwa kwa gharama kubwa na endapo wakibaini ,wawachukulie hatua za kisheria.
Amesema maeneo yote ya kutolea huduma, stendi, sokoni ,na maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu yawekewe vitakasa mikono na wale wote wanaokiuka maagizo ya wataalamu wa Afya wachukuliwe hatua, sambamba na wanaopotosha umma kuhusu ugonjwa wa corona wanachukuliwa hatua
“Minada na shughuli nyingine za kiuchumi ziendelee na wananchi wasitishwe kuhusu ugonjwa wa corona bali waendelee kupewa elimu kuhusu corona” .Alisema Mndeme
Maagizo mengine ni kuhakikisha maeneo ya stendi yanapuliziwa dawa kwakutumia magari na mabomba ya kupulizia dawa kwa mikono
Aidha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Jairos Khanga ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi ya janga la ugonjwa wa corona kwakuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya na kupuuza habari zinazosambazwa na mitandao ya kijamii nyingine zikiwa za upotoshaji.
Amesema kinga namba moja ni usafi wa mazingira yanayotuzunguka na kutakasa mikono mara kwa mara kwakutumia maji yanayo tiririka na sabuni, kutosogeleana, kupeana mikono sambamba na kutumia kiwiko cha mkono unapopiga chafya ili kuepuka maji maji yanayotoka puani au mdomoni kwenda kwa mwingine.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Mhe Oddo Mwisho ametoa rai kwa kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya na Mkoa kufanya ziara za kutembelea mipakani na kufanya ulinzi shirikishi lengo likiwa kukabiliana na wageni wanaoingia na kutok nchini kiholela ambao wanaweza kuleta athari za maambukizi zaidi
JACQUELEN CLAVERY
K /AFISA HABARI SONGEA DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa