Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi VijanaAjira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako (MB) leo 24/08/2023, ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha UfundiStadi na Marekebisho kwa Watu wenye ulemavu, kilichopo Kata ya Liganga, Halmashauri ya Wilaya yaSongea na kupongeza Jitihada zinazofanywa nawataalam katika kukamilisha mradi huo.
Mradi huu unatekelezwa kwa Awamu mbili, ambapoawamu ya kwanza utajumuisha ujenzi wamiundombinu ya vyumba na Madarasa (10) bwenilenye uwezo wa kuchukua wanafunzi arobaini (40) pamoja na nyumba moja yenye uwezo wa kuishifamilia tatu ( three in one). Mradi unatekelezwa kwanjia ya Force account na hadi kukamilika, ujenziutagharimu Tsh 1,000,000,000
Baada ya kupata Taarifa ya mradi kutoka kwaMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya yaSongea Ndg Neema Maghembe,Mh. Waziri alizunguka alizukunga kukagua kazi zinazofanywa na mafundi,pamoja na ubora wa majengo. Baada ya hapo Mh. Prof. Ndalichako, alipata nafasi ya kuzungumza na wadauwalikuwepo eneo hilo.
“Mkurugenzi nimepokea taarifa yako ambayo kwahakika imejieleza vizuri, jinsi mradi unavyotekelezwa.Lakini nimeona pia kazi inavyoendelea kwa hiyonikupongeze kwa kazi inavyofanyika, ambayoinafanyika kwa ubora na kwa kiwango kizuri, naaminikwamba mtaweza kuikamilisha kwa muda mliopanga”
Pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mtendajialitoa changamoto ambazo zimekuwa zikikwamishamradi kwenda kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kukosamaji, kutokana na chanzo cha maji kuwa mbali na eneola Mradi, kuongezeka kwa gharama za vifaa nagharama za usafirishaji kutoka eneo la mjini (sokoni)kuelekea eneo la kijiji ambapo mradi huounatekelezwa.
Akielezea changamoto hizo, Mh. Prof Ndalichakoalisema “ Changamoto mlizotoa nimezipokea, na nipona mkurugenzi anaeshughulika na maswala ya watuwenye Ulemavu, ambaye ndiye msimamizi mkuu wamradi huu, hivyo naomba hizo changamoto azipokeena ahakikishe anazifanyia kazi.”
Lengo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania ni kuhakikisha watu wenye Ulemavuwanapata fursa za kupata Elimu, na Mafunzo yaUfundi Stadi, Chuo hiki ni cha ufundi Stadi namarekebisho, hivyo lengo pia ni kuwafanyiamarekebisho ya kuwapunguzia makali ya ulemavu auMwenyezi Mungu akipenda, Ulemavu ukaondokakabisa hii ndio dhamira ya dhati ya Mh. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan
Aidha Mhe. Ndalichako alimpongeza, Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anazozifanya zakuleta maendeleo na mabadiliko makubwa katika nchi yetu katika Nyanja mbalimbali. ‘‘TumpongezeMheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Joakim Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kazi kubwaanayoifanya ya kuhamasisha wananchi kuletamaendeleo katika Jimbo la Peramiho’’.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa