Pongezi
Halmashauri ya Wilaya ya Songea imepongezwa kwa kutekeleza vizuri miradi ya maendeleo iliyopitiwa na mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2018
Pongezi hizo zimetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Bw Fransis kabeho wakati wakuhitimisha mbio hizo katika kijiji cha Sinai Manispaa ya Songea hivi karibuni.
Bw kabeho amesema Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni miongoni mwa Wilaya nne zilzotekeleza miradi ya maendeleo vizuri katika Mikoa 10 iliyopitiwa na mwenge wa uhuru 2018.
Bw kabeho amesema Serikali ya awamu ya tano inyoongozwa na Mh Raisi Dkt John Pombe Magufuli inadhamira ya dhati ya kueleta mabadiliko ya maendeleo kwa watanzania hivyo watendaji wa Serikali watekeleze wajibu wao kwakufanya kazi kulingana na taratibu zinazo takiwa na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.
Bw kabeho ameto wito kwa Watanzania kuendelea kuunga mkono jitihata za Mh Rais wa Jamumuhuri ya Muungano wa Tanzania kujitolea katika kutekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo serikali inatekeleza katika maeneo yao kama vile ujenzi wa miradi ya madarasa ,zahanati,nyumba za watumishi,miradi ya maji nk.
Mwenge wa Uhuru ni chachu ya kuleta maendeleo katika jamii hivyo unamtaka kila Mtanzania kufanya kazi kwa bidii,juhudi na maarifa.
Imeandaliwa na Jacquelen Clavery _Habari Mawasiliano na Mahusiano kazini.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa