Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaj wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jacob Mwambegele amefika Halmashauri ya Wilaya ya Songea leo tarehe 18/03/2024, kwa lengo la kuangalia namna maandalizi ya uchaguzi yanavyoenda.
Lengo la ujio wake ni kushuhudia maandalizi ya uchaguzi, na pia atakuwepo mpaka siku ya uchaguzi kujionea kila kitu kuanzia ufunguaji wa vituo, upigaji Kura na pia atashuhudia wakat wakihesabu kura katika vituo vyote vilivyopo kata ya Mbingamhalule siku ya tarehe 20/03/2024.
Akiwa Halmashauri alipokelewa na Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Peramiho Ndg. Khashim Lugome, na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mwl. Bumi Kasege, ambapo pamoja na mambo mengine alisema
“ Nimekuja kushuhudia maendeleo na maandalizi ya uchaguzi mdogo utakaofanyika tarehe 20/03/2024. Wote mnatambua kuwa kata ishirini na mbili zilizoko mikoa mbalilmbali nchini Tanzania zinategemea kuwa na uchaguzi siku hiyo. Hivyo mimi nimeamua kuja Songea kushuhudia maandalizi yanavyoenda, ambapo kwanza ntaangalia mafunzo yanayofanya na Wasimamiz wa vituo, pia ntatembelea vituo vyote vya kupigia kura na ntakuwepo mpaka siku ya uchaguzi ili kushuhudia kuanzia vituo vinavyofunguliwa mpaka wakati wa kuhesabu kura”
Naye Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Peramiho Ndg. Khashim Lugome, alimuhakikishia kuwa kila kitu kipo sawa kwanzia mafunzo vifaa vya kupigia kura pamoja na wafanyakazi watakaosimamia zoezi hilo. Lakini pia ulimuhakikishia uwepo wa usalama katika sehemu ya kupigia kura lakini pia kwa wagombea.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa