Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mhe. Mennas Komba umeutahadharisha umma kuhusu uharibifu wa vyanzo vya maji ambao unaendelea kutendeka katika jamii.
Mhe. Komba amesema uharibifu wa vyanzo vya maji ni hatari kwa ustawi wa viumbe hai vyote, hivyo wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu ambazo zinahatarisaha uhai wa vyanzo vya maji ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa viumbe na kazi zake.
“Nakuagiza Mkurugenzi kuwaandikia watendaji wote barua za kuwataka kubaini vyanzo vya maji bila kujali chanzo hicho ni cha mradi au hakina mradi kwa lengo la kulinda vyanzo hivyo”,amesisitiza Mhe. Komba.
Kwa upande mwingine Mhe. Komba amezitaka Mamlaka na wadau wa maji kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu na utunzaji wa vyanzo hivyo katika makazi yao.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa