Mwenge wa uhuru Kitaifa wapongeaza utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Mzee Mkongea Ali amepongeza utekelezaji wa ujenzi wa miradi iliyopitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019.
Mzee Mkongea Ali
amesema hayo wakati akikagua ,kuweka jiwe la msingi na kuzinduaa miradi mbalimba katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mzee Mkongea amesema miradi yote Ililiyojengwa na inayojengwa niwajibu wa kila mwananchi kuitunza na kuilinda kwa manufaa yetu na kizazi kijacho pia inajengwa kwa viwango vinavyotakiwa na kuzingatia miongozo inayotolewa na serikali.
“Uadilifu na uchapakazi ndio njia ya mafanikio yaTaifa letu, tufanye kazi kwa ajili ya kulijenga Taifa letu”.Amesema Mzee Mkongea Ali.
Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa umekagua miradi ya shamba la kahawa linalomilikiwa na kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa cha 842 JK, kisima cha mkono cha kupampu na mradi wa vishikwambi katika shule ya msingi Mapinduzi, umezindua mradi wa kisima cha asili kilicho boreshwa na kupanda miti rafiki ya maji, umefungua vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya mwalimu Mkuu katika shule ya msingi Lundusi na nyumba mbili za waganga katika Kijij i cha Parangu, mradi mwingine uliopitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ni ofisi za mthibiti ubora kwa shule za msingi ambapo uliweka jiwe la msingi.
Mwenge wa uhuru Kitaifa umekagua kuzindua , kufungua na kuweka jiwe la msingi jumla ya miradi saba yenye thamani ya zaidi shilingi milioni 762 na umekimbizwa kilomita 130.3
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa