MWENGE WA UHURU 2018
“ELIMU ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu’’. Ni kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru yenye ujumbe wakuitaka jamii kuwekeza katika Elimu kwa maendeleo ya Taifa.
Ujumbe huo umetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ndugu Fransis Kabeho siku ya kwanza ya mbio hizo wakati akimkabidhi mwenge huo mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Pololeti Mgema katika kijiji cha Liganga kata ya Liganga kwa ajili ya kukimbiza katika halmashauri ya wilaya ya Songea hivi karibuni.
Bw. Kabeho amesema wazazi/walezi waendelee kuwapa watoto wao mahitaji yote ya msingi ya shule kama vile sare za shule, viatu, madaftari na kuwachangia chakula mashuleni ili watoto waweze kusoma vizuri na kwa usikivu kwakuwa njaa huvunja usikivu kwa mwanafunzi kujifunza vizuri.
Aidha Bw kabeho amewataka watendaji wa serikali kutumia fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi zitumike kadiri ya miongozo inayotolewa na serikali na sio vinginevyo na miradi hiyo iweze kudumu kwa muda mrefu.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bw Fransis Kabeho amezindua, kuweka mawe ya msingi na kufungua miradi nane katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ikiwemo madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi liganga, nyumba moja ya mwalimu na matumizi ya Vishikwambi kijiji cha Mbinga Mhalule, uzinduzi wa kisima cha maji ya pampu kijiji cha matomondo, zahanati kijiji cha Lipokela miradi mingine ni uwekaji jiwe la msingi kwenye kiwanda kidogo kijiji cha Nakahegwa na maabara iliyopo katika shule ya Ukombozi.
Imeandaliwa na
Jacquelen Clavery. Habari Mawasiliano na Mahusiano Kazini
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa