Shirika moja lisilo kiserkali la J.I.S limetoa msaada wa baiskeli na kabati kwa viongozi wasimamizi wa watoa hudma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wagonjwa majumbani kwa kata 16 za Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mh Rajabu Mtiula katika Ofisi za Halmashuri ya Wilaya zilizopo kata ya peramiho kijiji cha Lundusi hivi karibuni.
Akikabidhi vifaa hivyo Mh Mtiula amewataka watoa huduma hao kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyo kusudiwa na sivinginevyo na endapo mtoa huduma atafanya hujuma yoyote kuhusu,upotevu, kuweka poni vifaa hivyo atambue sheria kali itachukuliwa dhidi yake.
Amesema Mtoahuduma anapo ona uovu wowote unatendeka katika jamii hususani kwa watoto watoe taarifa haraka sana katika vyombo vya dola kwa lengo la mamlaka zinahusika zifanye kazi yake, na mtoa huduma yoyote atakaye bainika kunyamazia maovu atachukuliwa hatua za kisheria pia.
Shirika la J.I.linatoa huduma ya kuwa wawezesha viongozi wanaowasimamia watoa hudumakwa wagonjwa na watoto wanaishi katika mazingira magumu kwakuwapa Elimuna vitendea kazi ili waweze kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuwasaida wagonjwa wanaishi na virusi vya UKIMWI.
Jumla ya baiskeli 16 na kabati 16 zimetolewa kwa kata zote 16 za Halmashauri ya Wilaya ya Songea.Tayari watoa huduma hao wlishapokea mafunzo kutoka kwenye shirika hilo namna ya kuwafutilia wagonjwa na kujua changamoto zao iliziweze kupatiwa uvumbuzi
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa