MRADI wa maji katika Kata ya Muhukuru Lilahi Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma umekamilika na umeanza kutoa huduma kwa wananchi
Diwani wa Kata ya Muhukuru- Lilahi Simoni Kapinga ameyasema hayo wakati anazungumza na wataalam wa Halmashauri hiyo mara baada ya kukagua mradi. .
Kapinga amesema kukamilika kwa mradi wa maji katika kata hiyo umesaidia kuongeza chachu ya maendeleo kama vile uandaaji wa matofari kwa ajili ya ujenzi wa nyumbani, kuboresha mazingira,kujiepusha na magonjwa ya matumbo na wanawake kutumia muda mwingi kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
“Bi Amina Juma ni mkazi wa kata hiyo anatoa shukrani kwa serikali kwasababu kwakipindi kirefu wamekuwa wakipata shida ya maji hivyo kukamilika kwa mradi huo umetupunguzia kero ya maji hasa sisi akinamama ambao tunatumia muda mwingi kupanga foleni ya kusubiri maji”,Alisema.
Kaimu mhandisi wa maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Jeremia Maduhu ametoa wito kwa wanachi wa kata hiyo ambao bado huduma ya maji haiijawafikia kujitolea kuchimba mitaro kwa ajili ya kutandika mabomba na mafundi waanze kuwafungia maji, pia ameeleza maji yapo ya kutosha kutoka kwenye chanzo kwenda kwenye tanki na kuwa fikia wananchi.
Amewaataka wananchi kutunza miundo mbinu ya maji kwasababu wa nufaika wa huduma ya maji ni wao,endapo watafanya hujuma yoyote ya kuhujumu miundo mbinu ni sawa na kijihujumu wenyewe na kuendelea kupata kero ya huduma hiyo.
Mradi wa maji unaotoa huduma katika kata ya Muhukuru –Lilahi unatekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa kushirikiana na wamisionari wa Abasia ya Hanga
JACQUELEN CLAVERY-K/ AFISA HABARI
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa