MPANGO na bajeti
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mhe .Menas Komba amewaagiza wakuu wa idara na vitengo kutumia kila mbinu kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaongezeka.
Komba ametoa maagizo hayo wakati akifunga mkutano maalum wa baraza la madiwani la kupitisha mpango na bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021 / 2022 uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Mhe. Komaba amesema wakuu wa idara na vitengo watumie kila mbinu pamoja na mpango kazi utakao onyesha mkakati wa ukusanyaji wa mapato kwa kila idara na kitengo.
Akiwasilisha mpango na bajeti ya maedeleo ya Halmashauri kwa mwaka 2021/2022-2023/2024 Afisa mipango wa Halmashauri hiyo Athumani Nyange amesema Halmashauri imekasimia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 28.1.
Nyange ametaja vyanzo mbali mbali vya mapato kuwa ni mapato ya ndani,mishahara,ruzuku toka serikali kuu na ruzuku ya miradi ya maendaleo.
Amesema kwa mwaka wa fedha huo Halmashauri imepanga kutumia fedha katika maeneo yasiyo ruzuku na ya ruzuku na miradi ya maendeleo .
Ameongeza kwakusema bajeti ya Halmashauri imeongezeka kutoka ukomo wa shilingi bilioni 22.2 hadi kufikia bilioni 28.1 sawa na ongezeko la asilimia 26.5 sababu ya ongezeko hilo kuwa ni ukomo wa bajeti ya mishahara na ukomo wa bajeti ya makusanyo ya mapato ya ndani.
Amevitaja vipaumbele vya bajeti ya mwaka 2021/2022 kuwa ni kukamilisha miradi viporo,kuajiri watumishi wapatao 784,kuboresha na kuendeleza usafi wa mazingira,kupambana na tatizo la lishe,ujenzi wa miundo mbinu ya elimu sekondari na msingi,kukamilisha ujenzi wa zahanati tisa na vituo vya afya vinne na hospitali ya wilaya pamoja na kutengeneza madawati na viti 500 kwa wanafunzi wa sekondari na msingi.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery Afisa habari
Songeadc
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa