Bi Elizabeth Gumbo ambaye ndie mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, apongeza kikundi cha vijana wa nguvu moja, ambao walipokea mkopo na kuanza kilimo cha Mahindi na Maparachihi.
Gumbo pia ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fulsa zinazotolewa na Serikali ili kujikwamua kimaisha
Ameyasema hayo baada ya kutembelea shamba la hekali saba linalomilikiwa na vijana Lugano wa kijiji ch nguvu moja ambapo katika shamba hilo, hekali tano wamelima mahindi na hekali mbili wamelima zao la maparachichi.
Vijana hapo walipata mkopo wa kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana ambayo ni 4% ya mapato ya ndani ya Halmashauri wenye thamani ya shilingi million saba( 7,000,000) hivyo wakaamua kuwekeza nguvu na akili kwenye kilimo ambacho ndo shughuli kubwa ya kikundi hicho.
“ Shughuli kubwa ya kikundi chetu ni kilimo cha Mahindi na Maparachichi. Mradi wa maparachichi tunautekeleza kwenye eneo la hekali 2 ambazo zinamilikiwa na kikundi”
Aidha Mkurugenzi Mtendaji alitoa pongezi kwa kikundi hicho kwa namna walivyojipanga na kilimo, lakini pia kwa ujasili wao wa kuaamua kuungana na kuchukua mkopo na kuwekeza kwenye kilimo. Ametoa wito pia kwa vijana, kutumia fursa ya mikopo inayotolea na Halmashauri kwa ajili ya kuendesha shughuli ambazo zinaweza kuwaletea kipato
Kikundi hicho kilianzishwa 07.01.2021, katika kijiji cha Nguvu moja kikiwa na wanachama watano (5) na kilisajiliwa tarehe 28.07.2022 na kupewa cheti cha utambuzi NA CBO/1331
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa