MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe amewataka waganga wafawidhi katika vituo vya kutolea huduma za afya watimize wajibu na kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Ameyazungumza hayo katika ukumbi wa mikutano wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Lundusi-Peramiho.
Amesema waganga wafawidhi wafanye kazi zenye matokeo ili kuondoa manung’uniko na malalamiko kwenye vituo hivyo pia amesisitiza Daktari anapopata dharula na kutoka ahakikishe anamuacha msaidizi ili wananchi waendelee kupata huduma.
‘’Ndugu zangu mimi nitumie fursa hii kuwataka mfanye kazi zenu kwa kujiamini, kwa kutumia busara zenu zote na hekima lakini yale mambo manne ya Serikali yazingatiwe ambayo ni Sheria, Taratibu, Kanuni na Miongozo’’, amesema Ndugu Neema.
Aidha amewapongeza kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika vituo vyao vya kutolea huduma za afya kama miradi ya tozo, uviko na mradi wa huduma endelevu za maji na usafi wa mazingira vijijini.-
Kwaupande wake Afisa Utumishi Ndugu Hashim Lugome amesisitiza wasimamizi wa vyanzo vya mapato vinavyohusiana na NHIF, CHF, na User fee kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha vyanzo hivi vinaingiza mapato kwa wakati.
‘’Zingatieni Sheria, Kanuni na taratibu kaa kituoni uhudumie wananchi pia nendeni mkasimame imara katika kutekeleza wajibu na kuwasimamia wasaidizi wenu kama inavyotakiwa’’, amesisitiza Ndugu Lugome.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa