MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe na timu ya wataalamu wamefanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza Kwa mwaka 2023.
Madarasa hayo yanajengwa kwa fedha zilizopokelewa kutoka Serikali kuu kiasi cha shilingi Milioni 200.
Ndugu Neema ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho kwa kuleta fedha hizo kwaajili ya kutekeleza ujenzi wa Vyumba vya madarasa.
Akizungumza katika ukaguzi huo amewaagiza mafundi viongozi wa ujenzi kuandaa mpango kazi wa ujenzi wa madarasa kuanzia siku ya kwanza hadi siku ya mwisho ambayo wanatarajia kumaliza.
Aidha Ndugu Neema amewataka walimu wa shule hizo kuwasimamia mafundi kwa ukaribu, kuwanunulia vifaa vyote vya ujenzi mapema ili ujenzi uweze kukamilika kwa wakati.
‘’Naomba niwasisitize sana kuhusu ushirikiano kati ya walimu, mafundi viongozi na kamati za ujenzi mshirikiane vizuri katika kutekeleza mradi huu pale ambapo mnaona kuna changamoto naomba mshirikishe Viongozi na timu ya wataalamu ili tujue tunatatua vipi hizo changamoto na ujenzi uweze kwenda vizuri’’, amesisitiza Ndugu Neema.
Shule walizotembelea kukagua vyumba vya madarasa na Shule ya Sekondari Muhukuru chumba kimoja,Magagura vyumba vitatu, Mpitimbi vyumba viwili, Kilagano vyumba viwili, Darajambili chumba kimoja na chumba kimoja na Lupunga chumba kimoja.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa