Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Bi Elizabeth Mathias Gumbo, jana 25.05.2024 aliwaaga rasmi wanafunzi wa Shule za Msingi waolikua kambi ya siku 15 kwanzia Tarehe 10.05.2024 hadi 25.105.2024 katika Halmashauri ya Wilayani Songea.
Wanafunzi hao ambao wanachiriki michuano ya UMITASHUMTA kwa sasa wanatoka kambi ya Wilaya na wanaeleke kambi ya Manispa kwa ajili kushiriki mashindano ya Umitashusmta kwa ngazi ya Mkoa.
Kabla ya kuagana nao, Bi Elizabeth alishiriki mbio ( Jogging ) zilizoanzia katika hosteli walipowekea kambi yao mpaka viwanja vya michezo ambapo ndipo walipokuwa wakifanyia mazoezi ya michezo mbalimbali.
Wanafunzi hao ambao wapo mia moja na kumi (110) Wasichana 55 na Wavulana 55, watashiriki michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu kwa Wavulana na Wasichana, Mpira wa Kikapu ( BasketBall), Mpira wa mikono Handbaall, Mpira wa Nyavu ( Netball)
“Leo tunakwenda kuhitimisha kambi yetu kwa ngazi ya Wilaya, sasa tunakwenda ngazi ya Mkoa na baadae tutaelekea kambi ya Taifa. Kwa kweli napenda kumshukuru sana Mhe. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kurudisha masomo ya michezo mashuleni ili kuimarisha Afya yetu ya Akili pamoja na ubongo. Lakini pia tunamshukuru kwa kuruhusu mashindano haya ya Umitashumta kutoka ngazi ya Wilaya na sasa yanenda ngazi ya Mkoa na baadae Taifa
Kwa upande wa walimu ambao wamekua wakiwafundisha wanafunzi hao ( Wanamichezo) wamemuhakikishia mkurugenzi kwamba watatetea Ubingwa wao lakini pia watarudi na Makombe ya Kutiosha
Mkurugenzi ameahidi zawadi kwa washiriki wote kama watachukua ubingwa wa mishuano hivyo, na kwa kukazia hilo amewapa washiriki wote Tracksuit na vitu vyote muhimu ambavyo wanahitaj ili watumie wakiwa kambi ikiwemo mchele Sukari unga nk
Amewataka walimu wote watakaokua na wanafunzi hao wahakikishe wasisitiza nidhamu kwa wanafunzi lakini pia kuhakikisha wanamichezo hao wasafi kwani nalo ni moja ya ushindani.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa