Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mwl. Neema M Maghembe amempongeza Mhe. Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka utaratibu mzuri wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara kwa Kila Mkoa na kila wilaya.
Ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi mbalimbali waliojitokeza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika 9 Disemba 2023 katika Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wananchi kutumia fulsa zilizopo kujikwamua kiuchumi ili kuendelea kuuenzi uhuru tulionao. Amesema
“ Labda niseme tu ndugu zangu tunapo adhimisha sherehe hizi tunatakiwa kutafakari maendeleo na hatua tuliyo piga toka tupate uhuru mpaka sasa lakini naamini kila mmoja wetu hapa ni shuhuda wa hatua za kimaendeleo tulizopiga mpaka sasa huhitaji kusimuliwa kila mmoja anaona, binafsi nampongea Mhe Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanania kwa juhudi anazozifanya katika kuwaletea maendeleo Watanzania, vilevile Nampongeza kwa kuchukua hatua hii ya kusema kila mkoa Uadhimishe siku hii kwenye mkoa husika hii inatoa nafasi kwenu ninyi wananchi kutafakari maendeleo yanayofanyika katika maeneo yenu. Nami nawaalika ndugu zangu wananchi kutafakari uhuru huu tulionao kwa kutumia fulsa zilizopo katika maeneo yetu ili kuondokana na hali duni za kimaisha”
Pia katika maadhimisho hayo yaliambatana na mijadala mbalimbali iliyowasilishwa na watoa mada ambapo wananchi waliojitokeza waliweza kuchangia mada hizo,ambapo kitengo cha maendeleo ya jamii kiliwasilisha mada iliyosema KATAA UKATILI KUWA SHUJAA ikiwa inalengo la kupinga ukatili wa kijinsia hivyo wadau mbalimbali walijitokeza na kusema namnagani ukatili unafanyika , maeneo yanayofanyika ukatili, watu gani wanafanyiwa ukatili na sehemu ambayo unaweza kuripoti ikiwa umefanyiwa ukatili.
Maadhimisho haya ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara yalikuwa na kaulimbiu isemayo “MIAKA 62 YA UHURU, UMOJA NA MSHIKAMANO NI CHACHU YA MAENDELEO YA JAMII YETU”
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa