Kiongozi wa Mbio za Mwenge maalum wa Uhuru 2021 Luteni Josephine Mwambashi amewataka viongozi na watendaji wa serikali wanaopewa dhamana ya kusimamia ujenzi wa miradi mbalimabali kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na wananchi wanapata huduma.
Luteni Mwambashi ametoa kauli hiyo katika Mbio za Mwenge maalum wa Uhuru katika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma zilizofanyika hivi karibuni.
Luteni Mwambashi amesema serikali imekuwa ikiungamkono jitihada za wanachi katika ukamilishaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali hivyo watendaji wanaopata dhamana ya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi watekeleze na wakamilishe miradi hiyo na wananchi waweze kupata huduma.
“Ndugu zangu nasistiza kwamba serikali yetu inatujali sana kwakuhakikisha kwamba tunapta huduma muhimu lakini pia kutuunga mkono ili tusikatishwe tamaa kwamiundombinu ambayo tuliyoianzisha”,amesisitiza Luteni Mwambashi.
Luteni Mwambashi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kulinda miundo mbinu ambayo imejengwa katika makazi yao ili iendelee kutoa huduma.
Awali akipokea Mwenge maalum wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amesema Mwenge wa Uhuru katika wilaya ya songea utakimbizwa takribani kilometa 205.8 zikijumuisha Songea, Manispaa na Madaba.
Mgeme ameongeza kwa kusema jumla ya miradi tisa yenye thamani ya shilingi zaidi ya bilioni moja na milioni 600 itazinduliwa,kukaguliwa,kufunguliwa na kuwekewa jiwe la msingi.
Mgema ameitaja miradi ambayo mwenge maalum wa uhuru umeipitia kuwa ni miradi ya Afya,Elimu,Maji ukaguzi wa kisima cha jadi na kukagua shamba la miti la mtu binafsi ambalo linatoa fursa za kichumi kwa wananchi.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery.
Afisa Habari Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa