Makisio ya Bajeti ya maendeleo 2019/2020
Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma imepitisha makisio ya bajati ya shilingi billioni ishirini na tano na milioni miatano kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020.
Afisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya Songea Richard Masesa amesema vyanzo vya mapato ya fedha hizo ni makusanyo ya mapato ya ndani,mishahara,ruzuku toka serikali kuu,na ruzuku ya fedha za miradi ya maendeleo.
Amesema Halmashauri inatarajia kutumia kiasi hicho cha fedha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo,maeneo ya ruzuku na yasiyo na ruzuku,aidha bajeti hiyo imepungua kwa asilimia 14.4 kwasababu ya ukomo wa bajeati ya maji kuondolewa.
Masesa ametaja vipaumbele vya bajeti kuwa ni kukamilisha miradi viporo,kuajiri watumishi 182,wakiwemo wakuu wa idara ya maji,afya,ujenzi na mipango,takwimu na ufuatiliaji,kuboresha na kuendeleza usafi wa mazingira,kupambana na utapia mlo,vipaumbele vingine ni ujenzi wa miundo mbinu ya elimu ya msingi na sekondari,ujenzi wa zahanati saba,kutengeneza madawati na viti kwa shule za msingi na sekondari pamoja na kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati
Amesema bajeti inaweza kuongezeka au kupungua kutokana na mchakato wa bajeti unavyo endelea hadi bunge litakapo tangaza bajeti ya serikali,mpango wa bajeti umeandaliwa kwa kuzingati sheria,miongozo na miongozo mbalimbali ya bajeti.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa