MAKABIDHIANO YA MRADI WA VISIMA VYA PAMPU YA MKONO
Mbunge wa jimbo la Peramiho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira,kazi,vijana,na watu wenye Ulemavu Mh Jenista Joackimu Mhagama amekabidhi mradi wa sima vya pampu ya mkono kwa Halmashauri ya Wilaya ya songea vyenye thamani ya shiligi bilioni 1 na milioni 700
Amekabidhi mradi huo hivi karibuni katika ofisi ya idara ya maji ya zamani ziLsizopo Halmashauri ya maspaa ya songea.
Mh Mhagama amesema mradi huo wa visima utatoa msaada mkubwa wa kutatua kero ya maji kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Ametoa wito kwa Mkuugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Songea Bw Simon Bulenganija kuhakikisha wanatunza mradi huo ili uweze kudumu na uendelee kutoa huduma kwa jamii.
Aidha mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw simoni Bulenganija amemshukuru Mh Waziri kwa jitihada kubwa anazozifanya za kuisadia jamii katika kutatua kero za wananchi ikiwemo kero ya maji na kuhaidi kuutunza vema mradi wa maji.
Mradi wa visima hivyo umefadhiliwa na shirika la Help for Underseverd Comminities (HUC) Shirika linalosaidia jamii isiyojiweza.
Imeandaliwa na;
Jacquelen Clavery
Habari, Mawasiliano na Mahusiano Kazini
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa