Washiriki wa mafunzo 224 kutoka Halmashauri ya Wilaya Songea mkoani Ruvuma wamepatiwa mafunzo ya siku moja kwa ajili ya kugawa dawa kwa magonjwa yasiyo pewa kipaumbele katika shule za msingi na jamii.
Mafunzo hayo yamefanyika hvi ikaribuni katika mji mdogo wa Peramiho
Mratibu wa wa Magonjwa hayo wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Dk. Scolastika Mapunda amewataka wananchi kutopuuza matumizi ya dawa hizo kwa sababu ni muhimu kwa kinga.
Amezitaja aina za dawa ambazo zitatolewa kwa wanafunzi ni albendaazole kwa ajili ya minyoo ya tumbo na mectizan kwa ajili ya ugonjwa wa usubi ambao ni tishio katika jamii.
Amewashauri wananchi wasiwazuie watoto wao kumeza dawa hizo wakati wa ugawaji wa dawa hizo kwa kuwa hazina madhara yoyote.
Jacquelen Clavery.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa