MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi Neema Maghembe amewataka wanafunzi wanaopatiwa mafunzo ya Sensa kusikiliza kwa makini na kwa weredi ili waende kuleta ufanisi katika kazi.
Mafunzo hayo yanaendelea kufanyika katika shule ya sekondari Maposeni Wilaya ya Songea ambayo yalianza tarehe 31 Julai 2022 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 18 Agosti 2022.
Pia mafunzo hayo yanajumuhisha wanafunzi 636 na Wakufunzi 23 ambayo yanatoa elimu kwa vitendo kwa Makarani 562, Wasimamizi wa maudhui 58 na Wasimamizi wa TEHAMA 16.
‘’Nawaomba msikilize kwa makini ili baada ya mafunzo mkafanye kazi kwa kufuata miongozo na maelekezo mnayopewa na Wakufunzi wenu ili zoezi la sensa lipate kufanikiwa’’, amesisitiza Bi Neema.
Kwaupande wake Mratibu wa Sensa Wilaya ya Songea Zainabu Mbaruku amewaomba Wakufunzi na wanafunzi hao waendelee kujitoa na kujituma muda wote wa mafunzo.
Aidha, amesema vitendea kazi kwaajili ya zoezi la Sensa vimepokelewa vikiwemo vishikwambi, peni, vichongeo, vifutio, pamoja na madaftari.
Sensa ya watu na makazi inatarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti 2022 ambayo itasaidia Serikali kupanga mipango ya kimaendeleo . Sensa ufanyika kila baada ya miaka kumi na Sensa ya mwisho ilifanyika mwaka 2022.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
09 Agosti 2022.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa