TANZANIA hufanya maadhimisho ya Uhuru tarehe 9 Desemba kila mwaka. Katika siku hiyo mwaka 1961, Tanzania wakati huo Tanganyika ilipata Uhuru kutoka kwa Uingereza.
Katika kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru Viongozi, Watumishi na Taasisi mbalimbali za Wilaya ya Songea walikutana katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwaajili ya kuelezea jitihada na mafanikio ya sekta mbalimbali yaliyofanywa na Serikali ya Tanzania ndani ya miaka 61 tangu Uhuru.
Akizungumza Mwalimu Juma Nyumayo ambae aliwasilisha mada ya Siasa na Uongozi amesema Kabla ya Uhuru Tanganyika ilitawaliwa na Waingereza ilipitia changamoto mbalimbali kama vile kunyongwa, kudharirishwa na kuteswa kama wanyama lakini baada ya Uhuru kupitia Vyama vya Siasa kama TANU chini ya Rais wa kwanza Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwaongoza Vyema Watanganyika kwa kushirikiana na Viongozi wengine ambao hawakuwaingiza Watanganyika tena kwenye vita kubwa.
Kwaupande wake Afisa Elimu Lucy Mbolu akiwasilisha mada ya Elimu na Afya katika Wilaya ya Songea amesema kabla ya Uhuru utoaji wa elimu ulikua na ubaguzi na taasisi za kutolea huduma za Elimu zilikua chache, kwa Wilaya ya Songea Shule za msingi zilikua 17 na Sekondari zilikua 2 lakini baada ya Uhuru Serikali ilihakikisha Watanzania wanapata Elimu ambapo hadi sasa Wilaya ya Songea ina jumla ya shule za msingi 205 na Sekondari 76.
Hatahivyo katika Sekta ya afya hospitali zilikua 2 na Zahanati chache lakini baada ya Uhuru Wilaya ina hospitali 3, vituo vya afya 17 na zahanati 75 pia Hospitali na vituo vingine vya afya vinaendelea na ujenzi.
Nae Mhandisi Mlavi akiwasilisha mada ya Miundombinu, Mawasiliano na Nishati amesema kabla ya uhuru hali ya barabara haikua nzuri hata katika kusafiri gharama kubwa zilikua zikitumika na muda mrefu watu walikua wanatumia wakiwa njiani lakini baada ya Uhuru hali ya Miundombinu imekua nzuri na hiyo imebadilisha hali ya Kiuchumi katika maeneo mengi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa