Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamepatiwa mafunzo elekezi ambayo yatawasaidia kuongeza uelewa,uwezo wa kusimamia na kuongoza katika utekeleza wa majukumu yao kazi.
Mafunzo hayo yamefundishwa na wakufunzi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ambacho kipo Jijini Dodoma,mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Pololeti Mgema akifungua mafunzo hayo amesema mafunzo hayo kwa madiwani jambo la msingi na la muhimu kwasababu yatawasaidia kuongeza uelewa katika nafasi zao za uwakilishi na utumishi kwenye maeneo yao ya utawala.
Amewataka madiwani hao kuzingatia kanuni,taratibu na sheri sanjari na kujenga ushirikiano baina ya watendaji na wananchi wanaowawakilisha kwa lengo la kutekeleza majukumu ya Serikali kwa umoja.
Moja ya madiwani walioshiriki mafunzo kutoka Kata ya Liganga Mhe. Filbert Soko amesema mafunzo hayo yamewaongezea uelewa wa kutamnbua kila mtu anatakiwa kufanyanini kwenye eneo lake na nafasi yake katika utumishi.
Kwa upande wake mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo Charles Matekele amewashauri madiwani hao kuzingatia miongozo na taratibu ambazo zitawasaidia kujiepusha na hoja za kiugaguzi ambazo zitaweza kusababisha kupata hati chafu au yenye mashaka katika swala la usimamizi mzuri wa fedha.
Mafunzo hayo yamejikita katika mada mbalimbali zinazogusa masuala mtambuka ya usimamizi na uendeshaji wa shughuli za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Baadhi ya mada hizo ni uongozi na utawala bora.
Halmashauri ya wilaya ya songea inajumla ya madiwani 24 kati ya hao 16 ni madiwani wa kata na madiwni sita ni wavitimaalum.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa