MADARASA
Shilingi milioni 113 zimetuka katika kujenga vyumba sita vya madarasa katika kata za Mpandangindo,Mpitimbi naLiganga kupitia mpango wa lipi kulingana na matokeo (EP4R).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Songea Bw Simon Bulenganija ametoa ufafanuzi huu ofisi kwake hivi karibuni.
Bw Bulenganija amesema fedha hizo zimetumika kujenga vyumba vya madarasa katika kata ya Mpitimbi shule ya msingi Humbaro vyumba viwili na shule ya Msingi Kilawalawa darasa moja,katika kata ya Liganga limejengwa darasa moja katika shule ya msingi Putire na Kata ya Mpandangindo yamejengwa madarasa mawili katika shule ya Msingi Mpandangindo.
Amesema sambamba na ujenzi wa madarasa hayo kila darasa litakuwa na madawati 15 sawa na wanafunzi 45 tayari madawati hayo yamesha nunuliwa isipokuwa shule ya msingi Kilawalawa
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw Simoni Bulenganija anatoa wito kwa wananchi kuilinda na kuitunza miradi yote ambayo ipo katika maeneo yao badala ya kuiachia serikali kutunza.
JACQUELEN CLAVERY-TEHEMA-HABARI
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa