Halmashauri ya Wilaya ya Songea kupitia kitengo cha usafi na mazingira kimefanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa lengo la kuhamasisha shughuli za usafi wa mazingira ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya siku ya usafi duniani itakayofanyika Tarehe 16/09/2023.
Halmashauri imechukua hatua hiyo baada ya Tanzania na duniani kote kwa ujumla wakiadhimisha wiki ya usafi duniani ambapo kitaifa maadhimisho haya yanafanyika jijini Dodoma, Hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Songea ipo katika maandalizi ya siku ya usafi duniani ambapo inaadhimisha kwa kuhamasisha jamii kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Akizungumzia taarifa hiyo Afisa mazingira wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea Makisio Chengula amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote ya vijiji 56 ambavyo kamati hiyo ya usafi wa mazingira itakuwa inapita kufanya ukaguzi kwa kushirikiana na serikali za vijiji ambapo amesema.
"Kuna maeneo mengi katika Halmashauri yetu ya Wilaya ya Songea yanazalisha taka ngumu na laini lakini watu wamekuwa wakiziacha taka hizo zinazagaa maeneo mbalimbali na kupelekea uchafuzi mkubwa wa mazingira kwahiyo Halmashauri tumeunda kamati Maalumu ambayo itasimamia shughuli za usafi wa mazingira"
"Katika kufanikisha Zoezi hili kuna maeneo tumeyawekea kipaumbele katika kufanya usafi huo ikiwemo eneo la Hospitali ya Wilaya ya Songea iliyopo Mpitimbi, Hospitali ya mission Peramiho, vituo vya Afya vya Magagura, Matimira, Muhukulu, Liganga na Kilagano na Zahanati zote, maeneo ya stendi ya mabasi ambapo kwa hapa tutafanya stendi mpya (Peramiho), maeneo yanayofanyika minada na maeneo ya Soko la Peramiho".( Namihoro). Hivyo niombe wananchi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kushiriki kufanya usafi na kutoa ushirikiano kwa kamati na Serikali za vijiji"
" Kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika Tarehe 16/09/2023 katika Kijiji cha Lundusi ambapo ni makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea hivyo tutahitimisha kwa kufanya usafi wa mazingira yote ya ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, hivyo niwaombe wananchi wa Kata ya Peramiho hususani Kijiji cha Lundusi na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi katika Kilele cha maadhimisho hayo Kinachotarajiwa kufanyika Tarehe 16/09/2023"
"Pia napenda kumshukuru Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea kwa kutuwezesha kufanikisha zoezi hili muhimu na la Kitaifa" Alisema Makisio Chengula Kaimu Afisa Mazingira Wilaya.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa