Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh Pololeti Mgema amewataka wananchi kutumia rasilimali ardhi kwa uzalishaji wa mazao kwa lengo la kuleta maendeleo.
Ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miche ya korosho uliofanyika katika kijiji cha Nakawale hivi karibuni katika Halmashauri ya wilaya ya Songea
Mh Mgema amewataka wananchi kutumia ardhi kwa uzalishaji wa mazao kwa lengo la kuleta maendelo katika jamii na Taifa na kuacha tabia ya uvivu na uzembe badala yake wajitume kufanya kazi kwavile hali ya hewa nzuri na ardhi yenye rutuba Halmashauri ya Wilaya ya Songea imejaliwa na ipo yakutosha.
Mh Mgema ameagiza kila mkulima anayelima zao la korosho kulima hekali mbili kwa kuanzia sawa nakupanda miche 54-60 kwa hekali hizo mbili kwa Naserikari kupitia wataalam wake wakilimo ipotayari kushirikiana na wakulima kuanzia hatua ya awali mpaka uzalishaji kwakuwapati maelekezo na ushauri kwa matokeo chanya.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw Saimoni Bulenganija ametoa wito kwa wakulima kuchangamkia fursa za maendeleo pindi zinapotokea badala ya kuona fursa hizo si za muhimu kwao kwa lengo la kuinua uchumi wao na Taifa
Halmshauri ya Wilaya ya Songea imeotesha miche ya mikorosho therathini elfu (30000) inayotosheleza kupanda ekali miatano ambayo itatolewa bure kwa wakulima wa zao hilo.Zao la korosho limebainika kustawi katika kata za Mhukuru,Maposeni na Lilahi katika Halmshauri ya Wilaya ya Songea.
Zao la korosho nimoja ya mazao yanayohimizwa na Serikali kwa kukuza uchumi wa Taifa na mazao mengi ni pamba, kahawa,tumbaku na chai.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa