Mwenge wa uhuru leo 10/06/2024, imeingia rasmi Halmashauri ya Wilaya ya Songea ukitokea Halmashauri ya WIlaya ya Namtumbo, ambapo uLipokelewa katika kijiji cha Lipaya kata ya Mpitimbi na kukagua, kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali iliyopo halmashaauri ya wilaya ya songea
Aidha kiongozi wa Mbio za mwenge Ngd. Godfrey Eliakim Mnzava amekagua miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Maji katika kijiji cha Lipaya. Mradi huo unaotekelezwa na Kampuni y a RJ MUSA CONSTRUCTION CO.LTD ambapo gharama za Mradi huo wa Maji uliopo kijiji cha Lipaya umegharimu kiasi cha shilingi 1,936,886,234.85.
Akiwa kwenye Mradi huo wa Maji Mhe Mkuu wa Wilaya Kabla ya kumualika kiongozi wa Mwenge kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi, alimshurukuru Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe Jenista Joakim Mhagama kwa jitihada zake katika kuibua mradi huu wa maji
“ kiongozi wa mbio za Mwenge, awali ya yote nitoe shukrani kwa Mbunge wa jimbo hili, Mhe. Jenista Mhagama. Mhe Mbunge ndie muanzilishi wa mradi huu akishirikiana na wananchi na walianzisha kwa Lita elf sabini na sita 76,000 ambapo sisi kama Serikali kuu tuliongezea lita laki moja baada ya kuona jitihada za mbunge. Baada ya kusema haya Mhe. Nikukaribishe useme neno ikiwa ni pamoja na kuweka jiwe la msingi
Nimefurahi kuona mradi huu wa maji unaendelea, nimefurahi pia kuona namna Wilaya yetu inaendelea kutekeleza miradi ya maji kwa Wananchi, malengo ya Dkt. Samia Suluhu Hassani ni kuona wananchi wanapata Maji safi na salama, lakini pia ya uhakika.
Baada ya kupokea taarifa tumekagua miundombinu yenyewe jinsi ambavyo mmetelekeza, lakini pia tumekagua nyaraka mbalimbali zinazoonesha matumizi ya fedha. Hivyo basi Mhe Mkuu wa Wilaya baada ya kupitia kila kitu ikiwa ni nyaraka pamoja miundombinu, Mwenge wa uhuru umelidhika ya kwamba kazi mmeifanya vizuri”
Kiongozi wa mwenge pia alifurahishwa na namna jinsi utaratibu wa manunuzi kupitia Mfumo wa NeST ulivyozingatiwa na baada ya kujilidhisha na mambo ya Msingi, Mhe. Godfrey Manzava alilidhia kuweka jiwe la msingi
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa