Mkuwa wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema ameagiza hatawavumilia Wevyeviti wa Vijiji na Vitongoji watakao kuwa wazembe katika kusimamia na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika maeneo yao ya kazi au wao kuwa sehemu ya migogoro.
Pololeti ametoa maagizo hayo katika hafla fupi ya kuwaapisha Wenyeviti wa Vijiji,Vitongoji,wajumbe wa Serikali ya Kijiji iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Maposeni katika Mji mdogo wa Peramiho hivi karibuni.
Pololeti amesema viongozi wasimamie na kuhamasisha shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa miundo mbinu ya shule, miradi ya maendeleo ambayo ipo katika maeneo yao ya utawala na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika kazi za kujitolea pale wanapotakiwa kujitolea pia hatawavumilia viongozi wazembe ambao wanasubiri kuhamasishwa kutekeleza majukumu yao.
“Hakuna mtu atakaye tuletea maendeleo tutayaleta wenyewe wananchi kwa kushirikiana na Serikali”alisema Pololeti.
Halmashauri ya wilaya songea ina Vijiji 56 sawa na wenye viti 56, ina Vitongoji 443 sawa wenyeviti 443 wa Vitongoji pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji.
Bw Waniwiki Shawa ni moja ya Wenyeviti wa Viijiji kutoka kijij cha LITOWA amesema yupo tayari kukabiliana na changamoto na kuzitafutia ufumbuzi kwakushirikiana na kamati yake ya Serikali ya Kijiji pamoja na wananchi na kusimamia shughuli za maendeleo katika Kijiji chake.
Awali akiwaapisha Viongozi hao Hakimu wa Mahakama ya mwanzao Happiness Shelembi amewashauri kulinda na kuangalia ukomo wa madaraka yao ,kwasababu baadhi yao wamekuwa wakikiuka ukomo wa madaraka yao na kutoa hukumu ambazo hazistahili kutolewa na wao kitendo kinacho kwenda kinyume na taratibu , kanuni na sheria za Nchi.
JACQUELEN CLAVERY –KITENGO CHA TEHAMA -HABARI
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa