Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Rumavu Hossana Ngunge amezitaka kaya masikini kuibua miradi itakayo imarisha uchumi wa wananchi na endelevu ambayo itanufaisha jamii nzima siyo walengwa tu tatika kipindi cha utekelezaji wa miradi ya TASAF awamu ya tatu kipindi cha pili cha mwaka 2021.
Ngunge amesema katika kipindi cha awali miradi iliyokuwa ikiibuliwa ilikuwa haiwanufaishi wananchi wote bali ilikuwa inamnufaisha mlengwa au kikundi cha walengwa wanao husika na huo mradi kitendo ambacho Serikali imekiona hakina tija katika kuimarisha uchumi wa wananchi.
“Miradi unayotakiwa kuibua ni miradi itakayo wanufaisha wananchi wote siyo walengwa tu”,amesisitiza Ngunge.s
Ngunge ameitaja baadhi ya miradi ambayo kaya hizo zinaweza kuibua ni pamoja na ujenzi wa vivuko vidogovidogo,kilimo cha mazao ya kimkakati,utengezaji wa barabara za vumbi na ukarabati wa visima vya jadi.
Ameongeza kwakusema zoezi la kuibua miradi ya kaya masikini limeanza Mei 17 ,2021 kwa Vijiji 32 ambavyo vilikuwepo kwenye mpango kuanzia awali na Vijiji 24 vinaendelea kufanyiwa uhakiki ili navyo viingizwe kwenye mpango wa kunusuru kaya masiki Nchini cha awamu ya tatu kipindi cha pili.
Ngunge ameyataja makundi ya walengwa wanaostahili kupata ruzuku kupita TASAF bila kufanya kazi kuwa ni kundi la wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 65 watoto chini ya miaka 18,akinamama wajawazito na wagonjwa.
Kaya zenye uwezo wa kufanya kazi zita wajibika kufanya kazi na kulipwa ujira wa shilingi 3000 kwa siku, ndani ya mwezi mmoja wanatakiwa kufanya kazi siku 10 na kipindi cha ukamishalishaji wa mradi ni miezi sita sawa na siku 60 za kazi.
Wakiongea kwaniaba ya wanakaya wenzao wanakaya wa Kijiji cha Mpitimbi (A) wamesema wanakubaliana na utaratibu na miongozo inayotolewa na serikali nao wapo tayari kufanya utekelezaji wake.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea inajumla ya Vijiji 56 ambavyo vyote vitaingizwa kwenye mpango baada ya zoezi la uhakiki kukamilika kwa Vijiji 24 kulingana na utaratibu wa Serikali wakutaka kuzifikia kaya masikini kwa asilimia miamoja katika awamu ya tatu kipindi cha pili cha 2021.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
SongeaDC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa