Walengwa wa kaya masikini wa halmashauri ya wilaya ya songea mkoani Ruvuma wameulalamikia utaratibu wa kulipwa fedha kwanjia ya mitandao ya simu na banki.
Wameto malalamiko hayo katika mkutano wa hadhara wa walengwa kaya masikini kwa lengo la kujadili changamoto za malipo uliofanyika katika Kata ya Muhukuru,Kijiji cha Muhukuru Barabarani hivi karibuni.
“Tunapenda utaratibu wa zamani uendelee badala ya huu wa sasa ambao haueleweki”,wamesisitiza walengwa hao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mohamed Hamis Nombo na Sanje Idd Kisomola wamesema baadhi ya walengwa hawezi kutumia mitandao ya simu kwa usahihi jambo linalowasababishia kukosa malipo na wakati mwingine kudhurumiwa fedha zao.
Wameongeza kwa kusema kutoka na hali ya uzee na kutokuwa na uwezo wa kutembea wamekuwa wakitoa namba zao za siri kwa watu wanaowaamini kuwachukulia malipo, badala yake wamekuwa wakiwazunguka kwakuchukua fedha hizo na kuzitumia kwa manufaa yao na kuwaacha walengwa wakitangatanga.
Kwa upande Mratibu wa TASAF wa Halmashauri hiyo Bi.Hossana Ngunge amesema utaratibu wa malipo kupitia mitandao ya simu na benk ulifikiwa baada ya walengwa wa kaya masikini kuzilalamikia kamati ya usimamizi za mpango kuwa zinawahujumu fedha zao.
Bi.Ngunge ameongeza kwa kusema katika kukabiliana na changamoto hiyo wamejipanga kutoa elimu ya jamii kuwaelisha walengwa juu umuhimu wa malipo kulipwa kupitia njia ya benki na mitandao.
Amezitaja baadhi ya faida za kulipa kupitia mitandao na benki ni pamoja na walengwa kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na kupanga bajeti ukilinganisha na kulipwa fedha mkoni ambako kunaoneka baadhi ya walengwa kutumia fedha hizo kinyume na malengo.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa